Atawadhe aliyetokwa na upepo baada ya kuamka usingizini?

Swali: Je, muislamu anapoamka kutoka usingizini na akataka kutawadha kwa ajili ya swalah au akatokwa na upepo tu, analazimika kujisafisha kwa maji au anatawadha bila kujisafisha kwa maji?

Jibu: Yule anayeamka kutoka usingizini na hakutokwa na mkojo, kinyesi, madhiy, wadiy wala manii analazimika kutawadha tu kwa ajili ya swalah. Hukumu ni hiyohiyo kwa yule ambaye ametokwa na upepo hana haja ya kujisafisha kwa maji. Bali analazimika kutawadha tu kwa ajili ya swalah.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/104)
  • Imechapishwa: 14/10/2026