Swali 2432: Nasikia baadhi ya watu wakisema kwamba kutumia Siwaak ndani ya msikiti haijuzu. Je, jambo hili ni sahihi?

Jibu: Siwaak ni Sunnah. Inasisitizwa kuitumia kila inapohitajika, kama wakati wa wudhuu´, swalah, kusoma Qur-aan, kubadilika kwa harufu ya kinywa na mfano wa hayo. Inajuzu kuitumia ndani ya msikiti na nje yake, kwa kuwa hakuna dalili inayokataza kuitumia ndani ya msikiti wakati kuna haja ya kuitumia. Jengine ni kutokana na ujumla wa Hadiyth isemayo:

“Lau nisingeogopa kuwatafutia uzito ummah wangu, basi ningewaamuru watumie Siwaak pamoja na kila swalah.”[1]

Hata hivyo haifai kuzidisha kuitumia mpaka kufikia kiwango cha kujitapisha akiwa ndani ya msikiti kwa kukhofia kwamba matapishi au damu vitatoka kwake na kuuchafua msikiti.

[1] Ahmad (02/399), Abu Daawuud (47) na wengineo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/109)
  • Imechapishwa: 14/10/2026