Mgonjwa wa pumu aruhusiwe kufanya Tayammum badala ya maji?

Swali: Kuna mwanamke ni mzee ambaye anafanya israfu katika kutawadha mpaka kufikia kiwango cha wasiwasi. Je, apewe fatwa ya kufanya Tayammum kwa sababu ya kukhofiwa afya yake, kwani amepatwa na pumu kutokana na kutumia maji mengi kwenye kifua na nguo zake?

Jibu: Hapewi fatwa ya kufanya hivyo. Bali anashauriwa na kuelekezwa kwenye kheri. Awe pamoja na mtu wa kumuongoza na kumkataza kufanya israfu.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 14/10/2026