Swali 5896: Wanatawadha kwa kutumia maji ya bwawa ambayo hukusanyika katika bwawa hili kutokana na maji ya mvua. Imeonekana ndani yake minyoo inayotembea katika maji yanayobaki baada ya watu kunywa, kwa kuwa kuwepo kwa minyoo hii ni dalili kwamba maji hayo yamekaa kwa muda mrefu katika bwawa. Je, inajuzu kutawadha kwa maji hayo?
Jibu: Ikiwa maji haya hayajabadilika ladha yake, harufu yake wala rangi yake kwa sababu ya najisi, basi kuwepo kwa minyoo iliyotokea ndani yake hakuyadhuru, kwa sababu haiwezekani kujikinga na jambo hilo. Kwa hiyo linasamehewa kwa sababu ya mashaka na inajuzu kutawadha kwa maji hayo.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/72)
- Imechapishwa: 14/10/2026
Swali 5896: Wanatawadha kwa kutumia maji ya bwawa ambayo hukusanyika katika bwawa hili kutokana na maji ya mvua. Imeonekana ndani yake minyoo inayotembea katika maji yanayobaki baada ya watu kunywa, kwa kuwa kuwepo kwa minyoo hii ni dalili kwamba maji hayo yamekaa kwa muda mrefu katika bwawa. Je, inajuzu kutawadha kwa maji hayo?
Jibu: Ikiwa maji haya hayajabadilika ladha yake, harufu yake wala rangi yake kwa sababu ya najisi, basi kuwepo kwa minyoo iliyotokea ndani yake hakuyadhuru, kwa sababu haiwezekani kujikinga na jambo hilo. Kwa hiyo linasamehewa kwa sababu ya mashaka na inajuzu kutawadha kwa maji hayo.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/72)
Imechapishwa: 14/10/2026
https://firqatunnajia.com/kutawadha-maji-ya-kisima-yaliyo-na-wadudu/