Swali: Ikiwa kuwa na umri mkubwa kuna fadhilah katika Uislamu, je, hilo halipingani na du´aa ya muislamu ya kumuomba Allaah asimrudishe katika umri wenye udhalili?
Jibu: Kuna tofauti kati ya kuwa na umri mkubwa na kufikia umri wenye udhalili. Umri wenye udhalili ni mtu kufikia hali ambayo anapoteza akili yake, anakuwa na ukichaa na kuropoka. Katika hali hii haandikiwi thawabu wala kuandikiwa dhambi. Ama kabla ya hapo, haingii katika umri wenye udhalili. Maadamu bado ana akili na fikira zake, basi anaandikiwa mema na mabaya na bado ni mwenye kuwajibika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba kinga dhidi ya kufikia umri wenye udhalili
Fadhilah ya umri mkubwa inakuwa kwa yule aliyesimama imara katika kumtii Allaah. Lakini ikiwa mtu ana umri mkubwa huku akiwa anapuuza mambo ya wajibu na kufanya yaliyoharamishwa, basi umri wake mkubwa haumsaidii kitu. Bali unaweza kumzidishia upotovu na ubaya juu ya ubaya wake. Basi tunamuomba Allaah atupe usalama na afya.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
- Imechapishwa: 14/10/2026
Swali: Ikiwa kuwa na umri mkubwa kuna fadhilah katika Uislamu, je, hilo halipingani na du´aa ya muislamu ya kumuomba Allaah asimrudishe katika umri wenye udhalili?
Jibu: Kuna tofauti kati ya kuwa na umri mkubwa na kufikia umri wenye udhalili. Umri wenye udhalili ni mtu kufikia hali ambayo anapoteza akili yake, anakuwa na ukichaa na kuropoka. Katika hali hii haandikiwi thawabu wala kuandikiwa dhambi. Ama kabla ya hapo, haingii katika umri wenye udhalili. Maadamu bado ana akili na fikira zake, basi anaandikiwa mema na mabaya na bado ni mwenye kuwajibika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba kinga dhidi ya kufikia umri wenye udhalili
Fadhilah ya umri mkubwa inakuwa kwa yule aliyesimama imara katika kumtii Allaah. Lakini ikiwa mtu ana umri mkubwa huku akiwa anapuuza mambo ya wajibu na kufanya yaliyoharamishwa, basi umri wake mkubwa haumsaidii kitu. Bali unaweza kumzidishia upotovu na ubaya juu ya ubaya wake. Basi tunamuomba Allaah atupe usalama na afya.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
Imechapishwa: 14/10/2026
https://firqatunnajia.com/kuoanisha-kati-ya-fadhilah-za-umri-wa-makamo-na-kinga-dhidi-ya-umri-wenye-udhalili/