Swali: Mwenye kumwambia baba yake ´ewe kafiri` ukafiri unamrudilia yeye mwenyewe…

Jibu: Hili halimuhusu baba yake tu. Akimwambia muislamu yeyote ´ewe kafiri` ilihali sio kafiri, maneno yake yanamrulia yeye mwenyewe – tunaomba kinga kwa Allaah. Vivyo hivyo akimwambia ´ewe khabithi`, ´Allaah akulaani` au mfano wa maneno kama hayo, ikiwa hastahiki hilo, maneno haya hayaendi patupu. Bali madhambi na khatari yake inamrudilia yeye mwenyewe, ni mamoja ikiwa atamwambia baba yake au mtu mwingine. Lakini hata hivyo akimwambia baba yake hivo ni khatari zaidi kwa sababu huku ni kuasi haki za wazazi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا

“Na wala usiwakemee; na waambie maneno ya heshima.” (17:23)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (2) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-16.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015