55. Du´aa ya kumuombea maiti wakati wa kumswalia

  Download

156-

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُمْ وَارْحَمْهُمْ، وَعَافِهِمْ وَاعْفُ عَنْهُمْ، وَأَكْرِمْ نُزُلَهُمْ، وَوَسِّعْ مُدْخَلَهُمْ، وَاغْسِلْهُمْ بِالْمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ، وَنَقِّهِمْ مِنْ الْخَطَايَا كَمَا نَقَّيْتَ الثَّوْبَ الأَبْيَضَ مِنْ الدَّنَسِ، وَأَبْدِلْهُمْ دَارًا خَيْرًا مِنْ دَارِهِمْ، وَأَهْلاً خَيْرًا مِنْ أَهْلِهِمْ، وَزَوْجًا خَيْرًا مِنْ زَوْجِهِمْ، وَأَدْخِلْهُمْ الْجَنَّةَ، وَأَعِذْهُمْ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ[ وَعَذَابِ النَّارِ]

 “Eee Allaah! Mghufurie na mrehemu, muafu na msamehe na mtukuze kushuka kwake [kaburini] na mpanulie maingilio yake na muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase na makosa kama Ulivyoitakasa nguo nyeupe kutokamana na uchafu, mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba  yake, jamaa bora kuliko jamaa zake, mke bora kuliko mke wake na mwingize Pepo na mlinde na adhabu ya kaburi na adhabu ya Moto.”[1]

157-

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لِحَيِّـنا وَمَيِّتِـنا وَشـاهِدِنا، وَغائِبِـنا، وَصَغيـرِنا وَكَبيـرِنا، وَذَكَـرِنا وَأُنْثـانا. اللهُـمِّ مَنْ أَحْيَيْـتَهُ مِنّا فَأَحْيِـهِ عَلى الإِسْلام، وَمَنْ تَوَفَّـيْتَهُ مِنّا فَتَوَفَّـهُ عَلى الإِيـمان، اللهُـمِّ لا تَحْـرِمْنـا أَجْـرَهُ، وَلا تُضِـلَّنا بَعْـدَهُ

“Ee Allaah! Msamehe aliyehai katika sisi na aliyekufa katika sisi, aliyepo na asiyekuwepo, wadogo wetu na wakubwa wetu, wakiume wetu na wakike wetu.  Ee Allaah! Ambaye utampa uhai katika sisi basi mpe uhai katika Uislamu na utayemfisha katika sisi basi mfishe juu ya imani.  Ee Allaah! Usitunyime ujira Wake na wala usitupoteze baada ya yeye kuondoka.”[2]

158-

اللهم إن فلان ابن فلان في ذمتك وحبل جوارك، فقه فتنة القبر، وعذاب النار، وأنت أهل الوفاء والحق، فاغفر له وارحمه، إنك الغفور الرحيم

“Ee Allaah! Hakika fulani mwana wa fulani yuko katika dhimma Yako na kamba ya ujirani Wako, hivyo basi mlinde na fitina ya kaburi na adhabu ya Moto – Wewe ndiye mtekelezaji na wa haki, basi msamehe na mrehemu, kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[3]

159-

اللهم عبدك وابن أمتك احتاج إلى رحمتك، وأنت غني عن عذابه، إن كان محسنا فزد في حسناته، إن كان مسيئا فتجاوز عنه

“Ee Allaah! Mja Wako na mtoto wa kijakazi Wako ni muhitaji wa huruma Yako Nawe ni mkwasi wa kumuadhibu. Kwa hivyo akiwa ni mwema basi mzidishie katika mema yake na akiwa ni muovu msamehe.”[4]

[1] Muslim (02/663).

[2] Abu Daawuud (320), at-Tirmidhiy (1024), an-Nasaa´iy (1988), Ibn Maajah (01/480) na Ahmad (02/368). Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah (01/251).

[3] Ibn Maajah. Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah” (01/251). Pia ameipokea Abu Daawuud (03/211).

[4] al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye (01/359). Tazama ”Ahkaam-ul-Janaaiz”, uk. 125 ya al-Albaaniy.

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 01/05/2020