56. Du´aa ya maiti ya mtoto mdogo wakati wa kumswalia

  Download

160-

أللَّهُمَّ أَعِذْهُ مِنْ عَذابِ الْقَبْرِ

”Ee Allaa! Mlinde kutokamana na adhabu ya kaburi.”[1]

Ni vizuri pia endapo atasema:

للهُـمِّ اجْعَلْـهُ فَرَطـاً وَذُخْـراً لِوالِـدَيهِ، وَشَفـيعاً مُجَـاباً، اللهُـمِّ ثَـقِّلْ بِهِ مَوازيـنَهُما، وَأَعْـظِمْ بِهِ أُجُـورَهُـما، وَأَلْـحِقْـهُ بِصَالِـحِ الـمؤْمِنـين، وَاجْعَلْـهُ في كَفـَالَةِ إِبْـراهـيم، وَقِهِ بِرَحْمَـتِكَ عَذابَ الْجَـحِيمِ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لإِسْلافِنَا، وَأَفْراطِنَا وَمَنْ سَبَقَنَاَ بِالإِيمَان

“Ee Allaah! Mjaalie awe ni mtangulizi, ujira, muombezi anayekubaliwa kwa ajili ya wazazi wake. Ee Allaah! Ifanye mizani yao iwe mizito na ukuze ujira wao kupitia mtoto huyu. Vilevile muunganishe na waumini wema waliotangulia na umjaalie awe katika ulinzi wa Ibraahiym (´alayhis-Swalaatu was-Sallaam) na umkinge kwa huruma Yako kutokamana na adhabu ya Moto. Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake. Ee Allaah! Wasamehe watangulizi wetu na wale waliotutangulia kwa imani.”[2]

161-

اللهُـمِّ اجْعَلْـهُ لَنا فَرَطـاً وَسَلَـفاً وَأَجْـراً

“Ee Allaah! Mjaalie awe ni mtangulizi wetu na [tupate] ujira.”[3]

[1] Sa´d bin al-Musayyib amesema:

”Niliswali nyuma ya Abu Hurayrah wakati alipokuwa akimswalia mtoto ambaye hajapatapo kufanya kosa maishani nikamsikia akisema… ” Hadiyth ameipokea Maalik katika ”al-Muwattwa´” (01/288), Ibn Abiy Shaybah katika ”al-Muswannaf” (03/217) na al-Bayhaqiy (04/9). al-Arnaauutw amesahihisha cheni ya wapokezi wake katika ukaguzi wake wa ”Sharh-us-Sunnah” ya al-Baghawiy (5/357).

[2] Tazama ”al-Mughniy” (03/416) ya Ibn Qudaamah na ”ad-Duruus-ul-Muhimmah Li’aamat-il-Ummah”, uk. 15 cha Shaykh ‘Abdul-Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz (Rahimahu Allaah).

[3] ”al-Hasan [al-Baswriy] alikuwa akimsomea mtoto al-Faatihah na akisema… ” al-Baghaawiy katika ”Sharh-us-Sunnah (05/357) na ’Abdur-Razzaaq (6588). al-Bukhaariy ameipokea kwa kuiwekea taaliki katika ”Kitaab-ul-Janaaiz (65) mlango wa ”Qiraa-at-ul-Faatihaah ’alaa al-Janaazah” (02/113).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 01/05/2020