21. Kuwapa watoto majina ya Maswahabah na waja wema

4- Majina ya waja wema waislamu. al-Mughiyrah bin Shu´bah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Walikuwa wakiitwa kwa majina ya Mitume wao na majina ya waja wema wa kabla.”

Ameipokea Muslim.

Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio waja walio wema zaidi katika Ummah huu na baada ya hapo wanakuja wale waliowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa na mtazamo wa kina katika hilo. az-Zubayr bin al-´Awaam (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa na watoto wa kiume kumi ambapo aliwapa baadhi ya majina ya mashahidi wa Badr: ´Abdullaah, al-Mundhir, ´Urwah, Hamzah, Ja´far, Musw´ab, ´Ubaydah, Khaalid na ´Umar.

Vilevile kuna waislamu wenye kuwapa watoto wao wa kiume majina ya makhaliyfah wane: ´Abdullaah, bi maana Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum). Kadhalika wamewapa watoto wao wa kike majina ya wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kadhalika.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 19
  • Imechapishwa: 18/03/2017