Jina bora la Mitume ni la Nabii na Mtume wetu Muhammad bin ´Abdillaah. Swalah na salaam ziwe juu yake na ndugu zake wote katika Manabii na Mitume.

Baada ya wanachuoni kukubaliana juu ya kujuzu kuitwa kwa jina lake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wametofautiana juu ya hukumu ya kukusanya kati ya jina lake na kun-ya yake: Muhammad na Abul-Qaasim.

Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Usawa ni kwamba inajuzu kuitwa kwa jina lake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), imekatazwa kuitwa kwa kun-ya yake. Baya zaidi ni kuitwa kwa majina yake yote mawili katika uhai wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haijuzu kuitwa kwa jina lake na kun-ya yake yote mawili.”[1]

Hapa kunafuata faida ya kushangaza:

Mtu wa kwanza kuitwa Ahmad baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa ni Ahmad al-Faraahiydiy al-Baswriy, baba wa al-Khaliyl. al-Khaliyl alizaliwa mwaka wa 100.

[1] Zaad-ul-Ma´aad (02/347).

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 18
  • Imechapishwa: 18/03/2017