Swali: Muislamu anayo haki ya kumkufurisha au kumfanyia Tabdiy´ kila ambaye atatumbukia katika kufuru au Bid´ah?

Jibu: Kuwa na haraka ya kuwahukumu watu na kuwakufurisha na kuwafanyia Tabdiy´, hili halijuzu isipokuwa kwa wanazuoni ambao wanajua mipaka ya kufuru, Bid´ah, kuritadi na sababu zake wanazijua wanazuoni. Hili ni jambo khaswa kwa wanazuoni. Haijuzu kwa yeyote kumuhukumu mwenzake Bid´ah, kufuru, shirki naye hajui vidhibiti vya Takfiyr, Tabdiy´ na ufuska.

Mtu anatakiwa kuuhifadhi ulimi wake. Kuna khatari akamwambia mtu ambaye siye, kwamba ni kafiri, mzushi, mpotofu au fasiki. Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) mesema:

“Yeyote atakayemwambia ndugu yake “wewe kafiri!” naye si hivyo, maneno yake yatarejea kwake.”

Maneno yake yatarejea kwakwe mwenyewe. Ni lazima kwa muislamu kuhifadhi ulimi wake na asiuache hovyo ukawa huru katika masuala kama haya. Ni jambo la khatari. Yanahitaji mtu kwanza asome na ajue vidhiviti ya Takfiyr, Tabdiy´, Tafsiyq na si kuongea kwa ujinga, hisia, hamasa au ghera. Anaweza kutumbikia katika makosa na maneno yake yakamrejea yeye mwenyewe. Masuala haya ni khatari sana. Na haya maneno ambayo ulisema katika kukufurisha watu, Tabdiy´ au Tafsiyq hayaachwi bure. Ikiwa wanastahiki hayo, yanaenda kwao. Na kama hawayastahiki basi yanakurejelea wewe. Ni juu yako kuuhifadhi ulimi wako katika masuala haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127359
  • Imechapishwa: 04/11/2022