Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah kuhusu migomo, maandamano na uchaguzi?

Jibu: Ni kuwafuata kichwa mchunga maadui wa Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtafuata nyayo za wale waliokuwa kabla yenu hatua kwa hatua, shibiri kwa shibiri, mpaka wakiingia shimo la mburukenge nanyi mtaingia. Wakasema: “E Mtume wa Allaah! Unamaanisha mayahudi na manaswara?” Akasema: “Kina nani wengine?”[1]

Ni kuwafuata kichwa mchunga maadui wa Uislamu. Hebu watutajie maandamano sahihi yaliyofanywa na Abu Bakr Haram. Hebu watutajie maandamano sahihi wakati wa ´Aliy bin Abiy Twaalib na wakati wa Mu´aawiyah. Hebu watutajie maandamano katika zama za Umawiyyah au zama za Banuul-´Abbaas. Yametoka kutoka kwa maadui wa Uislamu na wakayapokea al-Ikhwaan al-Muslimuun.

Ulinganizi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun ni janga. Kila kunapojitokeza kitu kutoka kwa maadui wa Uislamu wanakipokea, ni mamoja wanaposikia kunazungumziwa maandamamo au maigizo. Wanakipata rangi kila kitu kinachotoka kutoka kwa maadui wa Uislamu. Ima wakaja na shubuha au wakasema uwongo.

al-Qaradhwaawiy – Allaah aukate ulimi na midomo yake – anawahimiza wanawake kucheza maigizo. Ee Allaah! Mwangamize al-Qaradhwaawiy ambaye ameyaharibu au ameyapiga vita mambo mengi ya dini. Vinginevyo hawawezi kuleta dalili yoyote kutoka katika dini ya Allaah.

az-Zindaaniy anawahimiza wanawake wa kiyemeni kushiriki vikao vya Mashaykh wa Yemen.

[1] al-Bukhaariy (4356) na Muslim (2669).

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As’ilat-us-Salafiyyiyn bi Faransaa https://muqbel.net/articles.php?art_id=11
  • Imechapishwa: 04/11/2022