Swali: Ni ipi hali ya Muhammad Suruur na unapendekeza kusoma vitabu vyake na kusikiliza kanda zake?

Jibu: Alikuwa rafiki yetu. Ameshatutembelea hapa [Dammaaj] mara mbili au tatu. Kisha baadaye akafichuka na qadhiya ya vita vya Ghuba na kubadilikakubadilika kwake. Wakati mwingine anamsifu at-Turaabiy, mara nyingine anamsimanga. at-Turaabiy – Allaah anaupige uso wake kwenye mchanga – hastahiki kusifiwa. Nimeshamzungumzia katika kanda nyingi. Anawatukana baadhi ya wanazuoni na mifumo yao. Ni mwenye kujikweza kwa sababu ana wakati wa kutosha wa kusoma magazeti na majarida. Kwa hivyo mimi sipendekezi kusoma vitabu vyake wala kusoma vitabu vya wafuasi wake. Bali nakushaurini kujiweka mbali nao. Ni Hizbiyyuun. Hizbiyyah yao imethibiti. Nimewazungumza katika kanda nyingi na sitaki kukariri.

Wamewafarikisha Ahl-us-Sunnah. Wamemghuri Salmaan al-´Awdah na Safar na matokeo yake wakafungwa jela. Nakunasihi usiwakaribie Hizbiyyuun pasi na kujali ni al-Ikhwaan al-Muslimuun, kundi la Muhammad Suruur, Qutbiyyuun, watu wa jumuiya Hikmah au watu wa jumuiya ya Ihsaan. Wakimbie mbali kama unavyomkimbia mbali mtu mwenye ukoma au kama unavyomkimbia simba mpaka watubu kwa Allaah. Wakitubu kwa Allaah basi wao ni ndugu zetu.

Wamewakimbiza vijana mbali kusoma elimu yenye manufaa. Wananukuu majarida na taarifa za khabari za London na wanasema Yuusuf al-Qaradhwaawiy amemzungumza Shaykh Ibn Baaz. Naomba ulinzi kwa Allaah kutokamana na shaytwaan!  Mambo gani haya? Ni nani Yuusuf al-Qaradhwaawiy ukimlinganisha na Shaykh Ibn Baaz? Huyu masikini Yuusuf al-Qaradhwaawiy atazungumza kuhusu Shaykh Ibn Baaz? Ndugu! Kuweni makini na vitimbi vya Ahl-ul-Bid´ah! Wanawatukana Ahl-us-Sunnah. Utamjua mtu kuwa ni mzushi pale anapowasema vibaya Ahl-us-Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=6942
  • Imechapishwa: 04/11/2022