Sunnah kulala kwenye mikeka na kuacha magodoro?

Swali: Je, mtu anaweza kuchukulia kulala kwenye mikeka wakati wa sasa ni Sunnah?

Jibu: Hapana. Sio Sunnah. Ni jambo linakuwa kutegemea haja.

Swali: Yule ambaye ana uwezo lakini anatenga baadhi ya siku analala kwenye mikeka.

Jibu: Ni sawa kama anataka kujipa mazingatio, kuihesabu nafsi yake na kufanya mazoezi. Ni kwa njia ya kuifanyia hesabu nafsi na kuikumbusha hali za mafukara. Vinginevyo kama Allaah amemfungulia vizuri basi amshukuru Allaah. Ale katika vizuri:

يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ

“Enyi Mitume! Kuleni katika vizuri na tendeni mema – hakika Mimi kwa yale myatendayo ni Mjuzi.” (23:51)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22202/هل-النوم-على-الحصير-من-السنة
  • Imechapishwa: 04/11/2022