Swali: Baadhi ya wanazuoni wanapinga adhaana ya msikiti Mtakatifu kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Ee Bilaal! Unapoadhini punguza kasi kidogo, na unapokimu ongeza kasi kidogo.”

Baadhi wanaifanya adhaana kama Iqaamah kwa maana ya kwamba hawaipunguzi kasi.

Jibu: Sunnah ni kupunguza kasi katika adhaana na kuharakisha wakati wa kukimu. Hii ndio Sunnah. Waadhini wa msikiti Mtakatifu wanarefusha na hawakhafifishi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22200/هل-السنة-في-الاذان-الترسل-ام-الحدر
  • Imechapishwa: 04/11/2022