Mwanamke aliyekufa kabla ya kuolewa Peponi

Swali: Mwanamke anapokufa bila kuwa na mume na akawa miongoni mwa watu wa Peponi. Je, ataolewa na mmoja katika waumini?

Jibu: Hili linarejea kwa Allaah. Kila mmoja atapata kile anachokitamani Peponi. Watapata yale wanayoyaomba; wanawake kwa wanamme. Mwanamme atapewa kile anachokiomba na mwanamke atapewa kile anachokiomba. Wote watakuwa katika neema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22198/هل-من-ماتت-دون-زوج-تزوج-في-الجنة
  • Imechapishwa: 04/11/2022