Swali: Wanawake ndio wakazi wengi wa Motoni. Je, Peponi ndio wakazi wachache au wengi pia?

Jibu: Wakati alipoulizwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Kwa sababu mnakufuru wema na mnakithirisha kulaani.”

Ambaye atakuwa mkweli katika wao basi atapata Peponi. Kama alivosema (Jalla wa ´Alaa):

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللَّـهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ وَعَدَ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚوَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao; wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanasimamisha swalah na wanatoa zakaah na wanamtii Allaah na Mtume Wake – hao Allaah atawarehemu. Kwani hakika Allaah ni Mwenye nguvu kabisa, Mwenye hekima. Allaah amewaahidi waumini wanaume na waumini wanawake mabustani yapitayo chini yake mito ni wenye kudumu humo milele na makazi mazuri katika mabustani ya kudumu milele – na radhi kutoka kwa Allaah ndio kubwa zaidi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” (09:71-72)

Kila muumini wa kiume na muumini wa kike ameahidiwa kuingia Peponi. Kila kafiri wa kiume na kafiri wa kike ameahidiwa kuingia Motoni. Lakini wakati ilipokuwa kukufuru wema wa mume, matusi, laana na kutonyooka juu ya haki ndio wakawa wakazi wengi wa Motoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22197/لماذا-كانت-النساء-اكثر-اهل-النار