Anataka kuzikwa nyumbani kwa sababu ya Abu Bakr na ´Umar

Swali: Je, inafaa kwa mtu kuweka sharti pindi anapokufa azikwe ndani ya nyumba yake?

Jibu: Hapana. Akishurutisha hivo ni sharti batili. Azikwe kwenye makaburi ya waislamu na asizikwe katika nyumba yake.

Swali: Wanajengea hoja ni kwa nini Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) wamezikwa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Kwa sababu ni Maswahabah wenye sifa za kipekee. Kwa hivyo wakazikwa pamoja naye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo chumba chake ikawa ni makaburi ya wote watatu na yakawa ni makaburi maalum.

Swali: Sababu ya wao kufanya hivo?

Jibu: Kwa sababu ni Maswahabah zake wenye sifa maalum (Radhiya Allaahu ´anhuma).

Swali: Kwa hiyo hili ni jambo maalum kwao wawili?

Jibu: Ilikuwa Ijtihaad ya Maswahabah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22192/هل-يجوز-دفن-ميت-في-بيته-بناء-على-طلبه
  • Imechapishwa: 03/11/2022