Swali: Mimi ni kijana ambaye nina uwezo wa kuhiji na bado sijahiji ile hajj ya kwanza. Baba yangu ananikatalia kuhiji. Ni ipi hukumu ya kukaa kwangu na hukumu ya baba yangu kunikatalia hajj?

Jibu: Ni lazima kwake kuhiji hata kama baba yake atamkatalia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika si venginevyo utiifu unakuwa katika mema. Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Lakini amzungumzishe kwa njia iliyo nzuri kama kumwambia “ee baba yangu, mimi namshukuru Allaah kuona ni muweza na jambo hili ni faradhi kwangu na mtu kama wewe ulitakiwa unisaidie katika mambo ya kheri.” Vivyo hivyo atake msaada kutoka kwa baba zake wakubwa, ndugu zake au majirani zake wema mpaka baba yake aridhie. Akiendelea basi asimtii.

Lakini sidhani kama kuna muislamu ambaye atang´ang´ania katika jambo hilo ikiwa ndani yake kuna kheri. Hatong´ang´ania. Mwanawe ni muweza na anamkatalia kuhiji? Kitendo hichi hakifanywi na muumini. Kinafanywa na mtenda madhambi au kafiri. Lakini akiendelea kushikilia msimamo wake licha ya maneno mazuri na nasaha basi asimtii. Ahiji na wala hakuna vibaya kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3759/ماذا-يفعل-من-يمنعه-ابوه-من-حج-الفريضة
  • Imechapishwa: 02/06/2022