Swali: Je, ni lazima kwa mtoto kuwahudumia wazazi kwa hali zote au ni pale tu ambapo wanakuwa ni mafakiri?

Jibu: Wajibu wake ni yeye kutomuhitaji yeyote na kujitosheleza mwenyewe.

Swali: Je, ni wajibu kwa mtoto muislamu kumpa matumizi baba yake kafiri?

Jibu: Ndio, ni katika kumfanyia wema mzazi hata kama atakuwa kafiri:

وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا

“Wakikufanyia juhudi kwamba unishirikishe na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii. Lakini suhubiana nao kwa wema duniani.”[1]

Ni wajibu kumfanyia wema mzazi ingawa atakuwa kafiri. Kwa ajili hiyo anarudisha ule wema waliyomfanyia. Haijalishi kitu hata kama ni kafiri. Hata hivyo asimfuate katika dini yake:

وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا

“Wakikufanyia juhudi kwamba unishirikishe na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii.”

 Hata hivyo anatakiwa kumtekelezea wema.

[1] 31:15

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 12/10/2023