45. Ni misafara ipi ya kijeshi ilifanyika mwaka wa 2?

Swali 45: Ni misafara ipi ya kijeshi ilifanyika mwaka huo?

Jibu: Katika mwaka huohuo mwanzoni mwa mwezi wa Rajab, ´Abdullaah bin Jahsh na Wahajiri wanane walianza safari ya kijeshi na wakamuua Ibn-ul-Hadhwramiy. Kukashushwa kuhusiana na tukio hilo:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ

”Wanakuuliza kuhusu mwezi mtukufu na kupigana humo.”[1]

[1] 02:217

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 110
  • Imechapishwa: 11/10/2023