Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن جابر رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رجل للنبي صلى الله عليه وسلم يَومَ أُحُد: أَرَأيتَ إنْ قُتِلتُ فَأَيْنَ أَنَا؟ قَالَ: ((في الجنَّةِ)) فَأَلْقَى تَمَرَاتٍ كُنَّ في يَدِهِ، ثُمَّ قَاتَلَ حَتَّى قُتِلَ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

89 – Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: “Kuna mtu alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya vita vya Uhud: “Ee Mtume wa Allaah! Nambie nikiuliwa nitaenda wapi?” Akamwambia: “Peponi.” Yule mtu akatupa tende alizokuwa nazo mkononi mwake na halafu akapigana mpaka akauliwa.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna upupiaji wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) juu ya kutaka kujifunza mambo. Mtu huyu alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na inaonekana kana kwamba ilikuwa ndio mazowea yake. Hawachi fursa yoyote mpaka wanahakikisha wamemuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu kwa kufanya hivo wanafaidika elimu na matendo. Mwanachuoni mwenye utambuzi wa Shari´ah Allaah amemtunukia elimu. Kisha ukiongezea juu ya hapo akiitendea kazi, hii ni neema nyingine. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa namna hii; wanamuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu hukumu ya Kishari´ah ili waitendee kazi. Hili ni tofauti na yale waliyomo watu wengi leo ambapo wanauliza kuhusu mambo ya Shari’ah na hata wakiyajua hawayatendei kazi na kuyapuuza. Kana kwamba malengo yao ya elimu ni kutaka kujua tu. Kwa hakika hii ni khasara ilio wazi. Kwa sababu mwenye kuacha kufanya matendo baada ya kuyatambua, basi mjinga ni bora kuliko yeye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/27-28)
  • Imechapishwa: 11/10/2023