Swali: Kuna wanaosema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatoka katika umbile la uanaadamu pindi anapoteremshiwa Wahy. Je, maneno haya ni sahihi?

Jibu: Ni maneno batili. Haijuzu kusema juu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) jambo ambalo ndani yake lina kashfa. Anatoka katika umbile la uanaadamu! Anakuwa vipi sahihi? Je, anakuwa mwendawazimu? Anakuwa katika hali ipi? Kwa maana akitoka katika umbile la uanaadamu atakuwa vipi? Ni mwanaadamu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wala hatoki katika umbile la uanaadamu. Kusema kwamba Wahy unamtia uzito hili ni sahihi. Pale anapoteremkiwa na Wahy unamtia uzito:

إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا

”Hakika Sisi tutaweka juu yako kauli nzito.” (73:05)

Ni kweli kuwa upokeaji wa Wahy unamtia uzito. Ama kuhusu kwamba anatoka katika umbile la uanaadamu, haya ni maneno batili. Ni kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (2) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-16.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015