Swali: Mwanamke yuko na mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu na anataka kuhiji mwaka huu. Anataka kumwachisha kunyonya kwa ajili ya jambo hilo. Je, anapata dhambi yoyote?
Jibu: Amshauri mume wake. Hapana vibaya ikiwa hakuna madhara yoyote katika kumwachisha kunyonya. Hapo ni pale ambapo anakula na anaweza kula chakula kingine. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا
”Watakapotaka kumwachisha kunyonya kwa kuridhiana baina yao wawili na mashauriano, basi hapana dhambi juu ya wawili hao.”[1]
Ni lazima kwa mwanamke kushauriana na mume wake ikiwa anataka kumwachisha kunyonya kwa muda wa chini ya miaka miwili. Hapana neno ikiwa kumwachisha kunyonya hakumdhuru kitu.
[1] 02:233
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23330/هل-يجوز-فطام-الطفل-لاجل-الحج
- Imechapishwa: 28/12/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Inafaa mwanamke kujifunua mbele ya baba wa mume wa kunyonya?
Swali: Baba yangu wa kunyonya anazingatiwa ni Mahram kwa mke wangu? Ni kanuni ipi inayotumika katika unyonyaji? Jibu: Wanachuoni wengi wanasema baba wa kunyonya ni kama baba wa mke kinasabu. Maoni sahihi kwangu naonelea tofauti na hivyo. Pia ndio chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah). Anaonelea kuwa baba wa…
In "Mavazi ya mwanamke na ndugu zake wa kiume"
Kwa bahati mbaya amemuoa dada yake wa kunyonya
Swali: Kuna mwanaume amemuoa mwanamke na akazaa naye. Baada ya kitambo ikambainikia kuwa ni dada yake wa kunyonya. Wafanye nini sasa? Mtoto anasibishwe kwa nani? Jibu: Watoto watanasibishwa kwao wawili kwa sababu hii ni ndoa yenye utata. Ikithibiti kuwa wamechangia ziwa, basi wanatakiwa kutenganishwa. Watoto ni wa kwao kwa sababu…
In "Wanawake isiyofaa kuwaoa"

Udugu wa kunyonya wa watoto wa mama tofauti
https://www.youtube.com/watch?v=2A9p27wXIIw Swali: Mwanamke ana watoto wanne ambao kila mmoja ana mama yake. Na yule anayemnyonyesha ndio mtoto wake. Je, watoto hawa wawili huzingatiwa kuwa ni ndugu wa kunyonya pamoja na kutofautiana kwa mama zao? Jibu: Ndio. Huzingatiwa kuwa ni ndugu wa kunyonya hata kama kila mmoja ana mama yake.
In "Udugu na kuoana"