Kumwachisha mtoto kunyonya kwa ajili ya kwenda kuhiji

Swali: Mwanamke yuko na mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu na anataka kuhiji mwaka huu. Anataka kumwachisha kunyonya kwa ajili ya jambo hilo. Je, anapata dhambi yoyote?

Jibu: Amshauri mume wake. Hapana vibaya ikiwa hakuna madhara yoyote katika kumwachisha kunyonya. Hapo ni pale ambapo anakula na anaweza kula chakula kingine. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا

”Watakapotaka kumwachisha kunyonya kwa kuridhiana baina yao wawili na mashauriano, basi hapana dhambi juu ya wawili hao.”[1]

Ni lazima kwa mwanamke kushauriana na mume wake ikiwa anataka kumwachisha kunyonya kwa muda wa chini ya miaka miwili. Hapana neno ikiwa kumwachisha kunyonya hakumdhuru kitu.

[1] 02:233

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23330/هل-يجوز-فطام-الطفل-لاجل-الحج
  • Imechapishwa: 28/12/2023