Hekima ya wanaume kuhalalishiwa hariri sawa na vidole vinne

Swali: Ni ipi sababu ya kuhalalishwa hariri kiasi cha vidole visivyozidi vinne?

Jibu: Kwa sababu mtu anaweza kuhitajia kwa ajili ya kuweka kiraka, kitufe na kadhalika. Ni katika rehema ya Allaah. Haya ni katika wepesi wa Allaah (Jalla wa ´Alaa).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23327/ما-علة-تحليل-اربع-اصابع-في-الحرير
  • Imechapishwa: 28/12/2023