Kwa bahati mbaya amemuoa dada yake wa kunyonya

Swali: Kuna mwanaume amemuoa mwanamke na akazaa naye. Baada ya kitambo ikambainikia kuwa ni dada yake wa kunyonya. Wafanye nini sasa? Mtoto anasibishwe kwa nani?

Jibu: Watoto watanasibishwa kwao wawili kwa sababu hii ni ndoa yenye utata. Ikithibiti kuwa wamechangia ziwa, basi wanatakiwa kutenganishwa. Watoto ni wa kwao kwa sababu ni ndoa yenye utata.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (36)
  • Imechapishwa: 16/08/2023