Swali: Msichana wangu amekataa posa ya mposaji. Hoja yake eti anataka kukamilisha masomo yake ya chuo kikuu. Hivyo amekataa kuolewa kabisa. Je, nimuozeshe licha kukataa kwake au nimsubiri amalize masomo yake?

Jibu. Msubirie. Lakini hakikisha unamchunga na unamlinda kutokana na shari. Kwa sababu leo fitina ni nyingi. Hakikisha unamchunga na kumlinda mpaka akamilishe masomo yake. Lakini bora kwake ni yeye kuolewa. Kuolewa hakupingani na kusoma. Anaweza kumuwekea sharti mume wake amwache asome. Tatizo litakuwa limeondoka. Amwekee sharti akamilishe masomo yake. Hapo tatizo litakuwa limeondoka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (36)
  • Imechapishwa: 16/08/2023