Swali: Muislamu nje ya nchi ambaye anaswali na kufunga Ramadhaan. Lakini anafanya kazi ya kama dereva wa lori na anabeba pombe kwenda katika makampuni. Ni ipi hukumu ya kazi yake hii kwa sababu wengi katika wateja ni makafiri?
Jibu: Haijuzu kwake kufanya kazi hiyo kama ni muislamu. Haijuzu kwake kubeba pombe. Anaichafua nafsi yake kwa jambo hilo. Yeye ni muislamu. Allaah amemkirimu Uislamu. Milango ya riziki ni mingi. Atafuta riziki yake:
وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ
“Na yeyote yule atakayemtegemea Allaah, basi Yeye humtosheleza.”[1]
Atafute riziki kwa njia nyingine.
[1] 65:02-03
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (46)
- Imechapishwa: 14/09/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Kufanya kazi kwenye mgawaha wanapohudumia nguruwe na pombe
Swali: Nafanya kazi katika mgahawa ambapo mmiliki wake ni kafiri, kunapikwa vyakula vya Haramu - kama vile pombe na nyama ya nguruwe. Ipi hukumu ya kazi hii? Jibu: Tunachokunasihi ewe Muislamu ambaye unashahidilia ya kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, pamoja…
In "Kazi na ajira"
Kupunguza ndevu kwa sababu ya kazi
Kuna Muislamu katika nchi za magharibi anayehitajia kazi kutokana na shida alionayo yeye na familia yake; mama na baba. Ametafuta kazi sana kwa njia ya uandishi na kupiga simu kwa kiasi cha mara arubaini [pasina mafanikio yoyote]. Anafikiria kuwa hakubaliwi kwa sababu ya ndevu zake. Je, inajuzu kwake kuzifupisha kwa…
In "Ndevu na masharubu"
Kusafiri katika mji wa kikafiri kwa ajili ya kufanya kazi
Swali: Umesema kuwa haijuzu kusafiri kwenda katika miji ya kikafiri kwa lengo la utalii. Je, inajuzu kwa mtu kusafiri kwenda katika miji ya makafiri kwa ajili ya kufanyakazi na kutafuta riziki huko kwa miaka mingi? Jibu: Ndio, inajuzu. Ikiwa hakupata kazi katika mji wa Kiislamu, inafaa kwake kusafiri na kutafuta…
In "Kazi na ajira"