Hapa itafaa kuchukua pesa ya wengine

Swali: Je, anatekelezewa adhabu ambaye ni muhitaji na fakiri na hivyo akalazimika kuiba ili aweze kula yeye na watoto wake?

Jibu: Akihitaji chakula na kama hali atakufa, basi atachukua mali ya wengine kwa kile kiwango kitachombakizia uhai wake, kwa sababu hiyo ni dharurah. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

”… na ilihali ameshapambanua kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura.”[1]

Lakini baadaye amlipe kiwango hicho mwenye mali yake.

[1] 06:119

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (46)
  • Imechapishwa: 14/09/2024