Kufanya kazi kwenye mgawaha wanapohudumia nguruwe na pombe

Swali: Nafanya kazi katika mgahawa ambapo mmiliki wake ni kafiri, kunapikwa vyakula vya Haramu – kama vile pombe na nyama ya nguruwe. Ipi hukumu ya kazi hii?

Jibu: Tunachokunasihi ewe Muislamu ambaye unashahidilia ya kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, pamoja na hayo unafanya kazi ya kuhudumia nyama ya nguruwe na pombe n.k. Najikinga kwa Allaah kutokana na hilo. Je, humuogopi kweli Allaah katika nafsi yako? Na ukawa mwenye kutafuta riziki kwa njia nzuri na kujiweka mbali na mfano [wa kazi] kama hizi. Haikustahiki [kazi] kama hii ewe muislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=855
  • Imechapishwa: 03/10/2020