Swali: Ni upi uchi wa mwanamke mbele ya wanawake wenziwe?

Jibu: Sijui kwa upambanuzi uchi wa mwanamke mbele ya wanawake wenzake. Udhahiri wa Qur-aan ni kwamba anafaa mwanamke kuonyesha yale anayofaa kuwaonyesha ndugu zake wa kiume wasioweza kumuoa. Wanazuoni wetu (Rahimahu Allaah) wametaja kwamba inafaa kwa mwanamke kutazama mwili mzima wa mwanamke isipokuwa tu yaliyoko baina ya kitovu na magoti. Dalili yao juu ya hayo ni yale aliyopokea Muslim kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaume asitazame uchi wa mwanaume mwenzake, na wala mwanamke asitazame uchi wa mwanamke mwenzake.”[1]

[1] Muslim.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/266-267)
  • Imechapishwa: 23/05/2026