Mwanamke analazimika kwenda kwa daktari wa kiume

Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kwenda kwa daktari wa kiume wakati kunapokosekana daktari wa kike? Ni yepi inayofaa kwake kuyaonyesha?

Jibu: Hapana vibaya kwa mwanamke kwenda kwa daktari wa kiume wakati ambapo hakuan daktari wa kike, kama walivosema hayo wanazuoni. Inafaa kwake mwanamke kumuonyesha daktari wa kike yale yote anayohitaji kuyaangalia. Hata hivyo ni lazima awe pamoja na ndugu wa kiume na daktari asikae naye sehemu ya faragha. Kukaa faragha ni haramu na hili kwa ajili ya dharurah tu.  Wanazuoni wamesema kwamba kitendo hichi kinafaa kwa sababu uharamu wake ni wa sababu na jambo ambalo uharamu wake ni wa sababu basi linafaa wakati mtu anapolihitajia.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/288)
  • Imechapishwa: 23/05/2026