Swali: Imamu anapopita katika Suurah ambayo ndani yake kuna sijda ya swalah hasujudu. Je, kitendo chake ni sahihi?

Jibu: Ikiwa ni katika zile swalah za kusomwa kimyakimya ni sawa. Kwa sababu iwapo atasujudu atawashawishi waswaliji na kuwachanganya. Ama ikiwa ni katika zile swalah za kusomwa kwa sauti ya juu basi imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali na akapita katika Aayah yenye sijda akasujudu. Haitakikani kutoka nje ya mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imamu anatakiwa kuombwa dalili. Huenda wale watu wa kawaida walioko nyuma yake wakadhani kwamba sijda hii aliyoacha kusujudu ndani yake sio sijda. Matokeo yake wakaipita na wasisujudu. Kwa hivyo haitakikani kwa imamu katika swalah za kusoma kwa sauti ya juu anapopita katika Aayah ambayo ndani yake kuna sijda akaacha kusujudu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (377) http://binothaimeen.net/content/13366
  • Imechapishwa: 03/10/2020