Kuna Muislamu katika nchi za magharibi anayehitajia kazi kutokana na shida alionayo yeye na familia yake; mama na baba. Ametafuta kazi sana kwa njia ya uandishi na kupiga simu kwa kiasi cha mara arubaini [pasina mafanikio yoyote]. Anafikiria kuwa hakubaliwi kwa sababu ya ndevu zake. Je, inajuzu kwake kuzifupisha kwa kiasi cha kiganja?

Jibu: Hapana. Asitafuti riziki kwa kumuasi Allaah. Amche Allaah:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yeyote (yule) anayemcha Allaah; (basi Allaah) Atamjaalia njia (ya kutoka katika matatizo). Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii.” (65:02-03)

Asitafuti riziki kwa maasi kamwe, si kwa kunyoa ndevu zake, kuzifupisha na mengine. Ashikamane na Dini yake na amuombe Allaah. Allaah Atamfungulia mlango wa riziki yake kwa njia asiyoitarajia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (5) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-22.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015