Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma al-Faatihah juu ya roho ya maiti siku ile aliyokufa?

Jibu: Hili halina asli. Maiti hasomewi chochote katika Qur-aan, si al-Faatihah wala Suurah nyingine. Halikuthibiti. Kilichothibiti ni kumuombea Du´aa na kumtolea Swadaqah. Ikiwa unataka kumnufaisha maiti mtolee Swadaqah. Ikiwa unataka kumnufaisha maiti muombee msamaha na muombee Du´aa. Ama kufanya mambo yaliyozushwa, hili halijuzu na wala hayamfai kitu maiti.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (5) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-22.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015