Swali: Binamu yangu, ambaye kishaoa, amenitokea kuomba kumuoa msichana wangu na ana watoto saba na umri wake ni miaka arobaini. Mke wake, ambaye ni mama wa watoto wake ni binti ya binamu yangu, kwa maana yeye na mke wake wote ni binamu zangu. Mke wangu na msichana wangu wote wanakataa kabisa ndoa hii. Hata hivyo yeye ni mtu mwema katika dini na tabia. Nifafanueni, je, niwalazimishe mke wangu na binti yangu wakubali kumuozesha ilihali sababu ya kukataa ni tabia mbaya sana za mke wake na kuna khofu ya uchawi na fitina mbalimbali, na pia nisipokubali kumuozesha kutakuwa na kukatika kwa undugu?
Jibu: Huna haki ya kumuozesha isipokuwa kwa idhini yake, huna haki ya kumlazimisha binti yako juu yake, hata kama ni miongoni mwa watu bora, hata kama hana mke, huna haki ya kumlazimisha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke aliyeachika haolewi mpaka aombwe ruhusa na bikira haolewi mpaka aombwe idhini.” Wakasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Yeye huona haya.” Akasema: “Idhini yake ni kule kunyamaza kwake.”
“Bikira anaombwa idhini na baba yake na idhini yake ni kule kukaa kwake kimya.”
Kwa hiyo ikiwa atasema ”ndiyo” au atanyamaza, basi muozeshe. Ama kwa kumlazimisha, usimlazimishe, hata kama binamu yako atakukasirikia au atakukata. Yeye ndiye mwenye dhambi ikiwa atakukata kwa sababu hujamuozesha msichana wako kwa kumlazimisha. Wewe huna dhambi, yeye ndiye anayefanya maasi. Maana yake anataka umlazimishe binti yako juu yake, jambo ambalo halijuzu. Muozeshe kwa yule ambaye binti yako anaridhia miongoni mwa watu wema, ni mamoja awe ana wake au hana, ni mamoja awe mkubwa au mdogo. Ikiwa binti ameridhia na kukubali, basi hilo ndilo linalotakiwa. Ikiwa Allaah atamuongoza mama yake na akakubali, basi hilo ni bora zaidi. Mshirikishe mama yake na chukua sababu zitakazomfanya aridhike. Kwa sababu ikiwa mama yake haridhiki, anaweza kuharibu ndoa, anaweza kumchanganya msichana na huenda ndoa isidumu, kwa kuwa mara nyingi binti humfuata mama yake. Huenda leo akakubali, lakini kesho akabadilika kwa sababu ya mama yake. Lakini jitahidi usimuozeshe mpaka awe ameridhika na mama yake pia ameridhika. Ama ridhaa ya binti ni lazima. Ridhaa ya mama yake ni bora ikiwa itawezekana ili kuepusha matatizo kabla na baada ya ndoa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3247/حكم-ارغام-البنت-على-الزواج-ممن-ترفضه
- Imechapishwa: 12/10/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3247/حكم-ارغام-البنت-على-الزواج-ممن-ترفضه
Imechapishwa: 12/10/2026
https://firqatunnajia.com/anataka-kumlazimisha-binti-yake-kuolewa-na-binamu-kwa-kuchelea-udugu-usikatike/