Namna ya swalah ya maiti ni mtu analeta Takbiyr na anasoma al-Faatihah baada yake. Kisha mtu analeta Takbiyr ya pili na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kisha mtu analeta Takbiyr na kusema:
اللَّهُمَّ ,اغْفِرْ لِحَيِّنَا وَمَيِّتِنَا ,وَشَاهِدِنَا وَغَائِبِنَا ,وَصَغِيرِنَا وَكَبِيرِنَا ,وَذَكَرِنَا وَأُنْثَانَا,اللَّهُمَّ إنك تعلم منقلبنا ومثوانا ,مَنْ أَحْيَيْتَهُ مِنَّا فَأَحْيِهِ عَلَى الإِسْلامِ و السُنّةِ، وَمَنْ تَوَفَّيْتَهُ فَتَوَفَّهُ عليهما
“Ewe Allaah! Tusamehe walio hai miongoni mwetu na waliokufa miongoni mwetu, waliopo miongoni mwetu na wasiokuwepo miongoni mwetu, wadogo wetu na wakubwa wetu, wanaume wetu na wanawake wetu. Hakika Wewe unajua marejeo yetu na makazi yetu na Wewe ni Muweza wa kila jambo. Ee Allaah! Yule utakayemuweka hai miongoni mwetu, basi mfanye aishi juu ya Uislamu na Sunnah. Na yule utakayemfisha miongoni mwetu, basi mfishe juu ya hayo mawili.”[1]
اللهم اغفر له وارحمه وعافه واعف عنه وأكرم نزله ووسّع مدْخله واغسله بالماء والثلج والبرد ونقه من الخطايا كما ينقى الثوب الأبيض من الدنس، اللهم أبدله داراً خيراً من داره، وأهلاً خيراً من أهله وزوجاً من زوجه اللهم أدخله الجنة وقه فتنة القبر وعذاب النار، و افْسَحْ له في قَبْرِهِ و نَوِّرْ لَهُ فِيه
“Ee Allaah! Mghufurie na mrehemu, muafu na msamehe na mtukuze kushuka kwake [kaburini] na mpanulie maingilio yake. Muoshe na maji na kwa theluji na barafu. Mtakase na makosa kama Ulivyoitakasa nguo nyeupe kutokamana na uchafu. Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake na mume bora kuliko mke wake. Mwingize Pepo na mlinde na adhabu ya kaburi na adhabu ya kaburi na adhabu ya Moto. Mpanulie kaburi lake na umwangazie ndani yake!”[2]
Kisha ataleta Takbiyr na atatoa Tasliym moja upande wake wa kulia. Anyanyue mikono yake pamoja na kila Takbiyr.
Kile kilicho wajibu katika hayo ni kuleta Takbiyr zote, kisomo cha al-Faatihah, kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), du´aa ya chini kabisa ya aliye hai kumuombea maiti na kutoa salamu. Yule mwenye kupitwa na swalah ya maiti, basi humswalia kaburini mwake hadi mwezi mmoja. Ikiwa maiti hayupo katika mji, basi humswalia kwa nia.
[1] Ahmad (2/368), Abu Daawuud (3201), at-Tirmidhiy (1024), Ibn Maajah (1498) na al-Haakim (1/358), ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.
[2] Muslim (963).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 33-34
- Imechapishwa: 18/10/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 33-34
Imechapishwa: 18/10/2026
https://firqatunnajia.com/34-namna-ya-kumswalia-maiti/