33. Wakati Mtume alipoashiria kwa ncha ya kidole chake kidogo

71 – Ahmad bin Muhammad bin ´Umar al-Warraaq ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal ametuhadithia: Muhammad bin Abiy Bakr al-Maqdamiy ametuhadithia: Huraym ametuhadithia: Muhammad bin Sawaa ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas, ambaye ameeleza:

”Kwa mnasaba wa maneno Yake:

فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا

“Basi Mola wako alipojidhihirisha katika jabali, akalifanya livurugike kuwa vumbi.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaashiria kwa ncha ya kidole chake kidogo.”[1]

Hadiyth hii ni yenye kutambulika na imesimuliwa kupitia njia nyingi kutoka kwa Anas bin Maalik.

[1] Jaamiy´-ul-Bayaan (10/428-430).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 88-89
  • Imechapishwa: 18/10/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy