Inajuzu kuswali swalah ya khofu kwa namna yoyote miongoni mwa namna ambazo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali. Namna iliyochaguliwa miongoni mwa hizo ni kwamba imamu awagawe katika makundi mawili: kundi moja lilinde, na kundi lingine liswali pamoja naye Rak´ah moja. Atakaposimama kwenda Rak´ah ya pili, kundi hilo linanuia kujitenga naye na linakamilisha swalah yake, kisha linaenda kulinda. Kisha kundi lingine linakuja na kuswali pamoja naye Rak´ah ya pili. Atakapokaa katika Tashahhud, kundi hilo litasimama na kuswali Rak´ah nyingine. Naye atasubiri mpaka wafanye Tashahhud, kisha atatoa salamu pamoja nao.

Khofu inapokuwa kubwa, basi wataswali wakiwa wanatembea kwa miguu au wamepanda juu ya vipando, ni mamoja wameelekea Qiblah au kwengine, na huku wakiashiria kwa kurukuu na kusujudu.

Vivyo hivyo kila mwenye kuchelea juu ya nafsi yake ataswali kulingana na hali yake. Atafanya kila jambo analohitaji kulifanya, kama kukimbia au jambo jingine.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 30
  • Imechapishwa: 18/10/2026