Ikiwa umbali wa safari yake ni Farsakh 16 – nao ni mwendo wa siku mbili kwa safari ya kawaida – na safari hiyo ni ya halali, basi anaruhusiwa kufupisha zile swalah za Rak´ah nne pekee. Isipokuwa akiwa nyuma ya imamu mkazi, ikiwa hakunuia kufupisha, akasahau swalah ya akiwa mkazi ambapo akaikumbuka akiwa safarini au akasahau swalah ya safarini kisha akaikumbuka akiwa mkazi, katika hali hiyo ni juu yake kuswali kwa kukamilisha.
Msafiri anaruhusiwa kuswali kwa kukamilisha, ingawa kufupisha ndio bora.
Mwenye kunuia kukaa mahali zaidi ya siku 21, basi ataswali kwa kukamilisha. Ikiwa hakukusudia kukaa muda maalum, basi ataendelea kufupisha daima.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 30
- Imechapishwa: 18/10/2026
Ikiwa umbali wa safari yake ni Farsakh 16 – nao ni mwendo wa siku mbili kwa safari ya kawaida – na safari hiyo ni ya halali, basi anaruhusiwa kufupisha zile swalah za Rak´ah nne pekee. Isipokuwa akiwa nyuma ya imamu mkazi, ikiwa hakunuia kufupisha, akasahau swalah ya akiwa mkazi ambapo akaikumbuka akiwa safarini au akasahau swalah ya safarini kisha akaikumbuka akiwa mkazi, katika hali hiyo ni juu yake kuswali kwa kukamilisha.
Msafiri anaruhusiwa kuswali kwa kukamilisha, ingawa kufupisha ndio bora.
Mwenye kunuia kukaa mahali zaidi ya siku 21, basi ataswali kwa kukamilisha. Ikiwa hakukusudia kukaa muda maalum, basi ataendelea kufupisha daima.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 30
Imechapishwa: 18/10/2026
https://firqatunnajia.com/28-swalah-ya-msafiri/