25. Nyakati ambazo imekatazwa kuswali ndani yake

Ni nyakati tano:

1 – Baada ya Fajr mpaka jua lichomoze.

2 – Baada ya jua kuchomoza mpaka linyanyuke kiasi cha urefu wa mkuki.

3 – Wakati jua linapokuwa katikati ya anga mpaka lipinduke.

4 – Baada ya ´Aswr mpaka jua likaribie kuzama.

5 – Jua linapokaribia kuzama mpaka lizame.

Hizi ndizo nyakati ambazo haiswaliwi swalah ya kujitolea, isipokuwa katika kurudia swalah ya mkusanyiko ikiwa kumekimiwa swalah naye mtu yuko ndani ya msikiti, Rak´ah mbili za Twawaaf baada yake, swalah ya jeneza na kulipa zile swalah zinazopendeza zinazoswaliwa kwa mnasaba wa swalah za faradhi katika nyakati mbili miongoni mwa hizo, nazo ni baada ya Fajr na baada ya ´Aswr. Aidha inajuzu kulipa swalah za faradhi katika nyakati zote.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 28
  • Imechapishwa: 12/10/2026