Sahau katika swalah kuna aina tatu:
1 – Kuongeza kitendo cha aina ya swalah, kama kuongeza Rak´ah au nguzo. Swalah inabatilika kwa kufanya hivyo kwa makusudi. Akifanya hivo kwa kusahau, atasujudu sijda mbili za kusahau. Akijua akiwa katika Rak´ah ya ziada, hukaa mara moja. Ikiwa ametoa salamu akiwa amepunguza kitu katika swalah yake kisha akakumbuka baadaye, hufanya kile kilichobaki kwake katika swalah hiyo, halafu husujudu sijda ya kusahau.
Ikiwa atafanya jambo ambalo si la aina ya swalah, basi makusudi na kusahau kwake ni sawa. Ikiwa ni jambo kubwa, linabatilisha swalah. Ikiwa ni jambo dogo – kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipombeba Umaamah[1] na alipomfungulia ´Aaishah mlango[2] – basi hapana neno.
2 – Upungufu, kama kusahau wajibu. Yule mwenye kusahau Tashahhud ya kwanza na akakumbuka kisha akakumbuka kabla hajasimama sawasawa, anarudi na kuileta. Ikiwa amesimama sawasawa, harudi.
Ikiwa atasahau nguzo, kisha akakumbuka kabla ya kuanza kusoma katika Rak´ah nyingine, anarudi na kuileta, pamoja na vile vinavyofuata baada yake. Ikiwa atakumbuka baada ya hapo, Rak´ah ambayo aliacha nguzo hiyo ndani yake inabatilika.
Ambaye atasahau Sujuud moja kutoka katika zile Rak´ah zote nne na akaikumbuka katika Tashahhud, atasujudu papo hapo. Hapo Rak´ah moja itakuwa imekamilika kwake, kisha ataleta Rak´ah tatu.
3 – Shaka. Anaposhuku kuhusu kuacha nguzo, basi hukumu yake ni kama kwamba ameiacha. Yule mwenye kushuku kuhusu idadi ya Rak´ah, basi atajenga juu ya yakini, isipokuwa imamu pekee; yeye atajenga juu ya kile ambacho dhana yake kubwa inampelekea.
Kwa kila kilichosahauliwa kina sijda mbili kabla ya salamu, isipokuwa yule aliyetoa salamu akiwa amepunguza katika swalah yake, imamu anayejenga juu ya dhana yake kubwa na mwenye kusahau kusujudu kabla ya salamu. Huyu atasujudu sijda mbili baada ya salamu yake, kisha atafanya Tashahhud na kutoa salamu.
Maamuma hana sijda ya kusahau, isipokuwa imamu wake akisahau, basi atasujudu pamoja naye. Imamu akisahau au akapatwa na kitu, basi wanaume watamzindua kwa Tasbiyh na wanawake watamzindua kwa kupiga makofi.
[1] al-Bukhaariy (516) na Muslim (543).
[2] Abu Daawuud (922), at-Tirmidhiy (601), aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na ngeni, na an-Nasaa’iy (1207).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 26-27
- Imechapishwa: 12/10/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 26-27
Imechapishwa: 12/10/2026
https://firqatunnajia.com/23-sijda-ya-kusahau/