Mambo yake ya wajibu ni saba:

1 – Takbiyr nyingine zote isipokuwa Takbiyr ya kufungulia swalah.

2 – Mtu kusema katika Rukuu´ mara moja:

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

na kusema mara moja katika Sujuud:

سبحان ربي الأعلى

“Ametakasika Mola wangu Aliye juu kabisa.”

3 – Mtu kusema:

سَمعَ الله لِمنْ حَمِدَه

“Allaah amemsikia mwenye kumuhimidi.”

na:

رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ

“Mola wetu! Himdi zote ni Zako!”

wakati wa kuinuka kutoka katika Rukuu´.

4 – Mtu kusema:

رَبِّ اغْفِرْ لِي

“Mola! Nisamehe!”

baina ya Sujuud mbili.

5 – Tashahhud ya kwanza.

6 – Kukaa kwa ajili ya Tashahhud ya kwanza.

7 – Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Tashahhud ya mwisho.

Hizi akiziacha kwa makusudi, basi swalah yake inabatilika. Akiziacha kwa kusahau, basi atasujudu sijda ya kusahau. Mengine yaliyo nje ya hayo ni mambo yanayopendeza; swalah haibatiliki kwa kuyaacha kwa makusudi na wala si lazima kusujudu kwa kuyasahau.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 26
  • Imechapishwa: 12/10/2026