Sio kila mtu ana haki ya kujibu maswali

Swali: Ni wanachuoni wepi ambao inatakikana kusoma kwao? Je, inatosheleza kwa mtu kusoma muda mfupi ili astahiki kutoa fatwa na kusomesha?

Jibu: Anaweza kusoma miaka mia na asiwe ni mwenye kustahiki kutoa fatwa. Haihusiani na muda. Inahusiana na uelewa. Amepata uelewa? Amepata elimu? Hili linaweza kupatikana hata kwa muda mfupi. Huenda akajifunza kwa muda mfupi. Huenda asijifunzi kitu kwa muda mrefu. Haihusiani na muda mrefu wa kusoma. Inahusiana na uelewa. Hakuna mwenye kutoa fatwa isipokuwa tu yule mwenye uelewa katika Dini. Atoe fatwa wakati wa dharurah, ikiwa hakuna ambaye ni bora na ni mjuzi kuliko yeye. Fatwa ni jambo la khatari. Fatwa ni kumwelezea Allaah ya kwamba Amehalalisha au Kuharamisha kadhaa. Ndio maana Ibn-ul-Qayyim amekipa jina kitabu chake “A´laam-ul-Muwaqqi´iyn ´an Rabb-il-´Aalamiyn”. Anaashiria ya kwamba wale wenye kutoa fatwa wanaandika kwa niaba ya Allaah. Fatwa sio jambo sahali. Hatoi fatwa isipokuwa yule aliye na elimu iliyozama kabisa. Ama yule mwenye kufikiri tu au anasema jinsi huyu na yule amevosema, asitoe fatwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2025-12-1435.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015