Swali: Nina ndugu fakiri nje ya mji huu. Ameniomba kiwango cha pesa ili anunue ardhi alime miraa. Hivyo nikawa nimemkatalia kumtumia pesa. Je, nimefanya sahihi?

Jibu: Ndio. Lau ungelimtumia pesa ili anunue ardhi apande mirungi ungelikuwa umemsaidia katika madhambi. Mirungi ni haramu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ

“Saidianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Mirungi na sigara ni haramu kwa kuwa vinaua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kila chenye kulevya na kuua. Miraa ni mbaya zaidi kuliko sigara. Inaufanya moyo kupumzika. Umefanya jamb la sawa pindi ulipokataa kumuazima pesa ndugu yako anunue ardhi ambayo anafikiria kupanda miraa. Ni kwa nini asipande tende, mizabibu na vitu vingine ambavyo ni halali?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2025-12-1435.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015