Kumwacha mama mgonjwa kwa ajili ya masomo?

Swali: Muulizaji huyu ni kutoka Ubelgiji. Nataka kwenda kutafuta elimu. Lakini hata hiyo mama yangu ni mgonjwa na nina dada wawili wadogo. Je, nimwache mama yangu ambaye ni mgonjwa na niende kutafuta elimu au nibaki naye?

Jibu: Baki naye. Maadamu anakuhitajia baki naye na umhudumie. Haki zake ni zenye kutangulia hata kabla ya Jihaad katika njia ya Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimrudisha mtu kwa wazazi wake na kumwambia:

“Kapambane nao.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2025-12-1435.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015