Swali: Ni ipi hukumu ya picha kwa kutumia camera ya simu kwa kuwa baadhi ya watu wanasema kuwa ni kivuli tu na hilo halina uharamu wowote? Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Haina uharamu wowote kwake yeye. Ama kwa mujibu wa Sunnah na dalili picha zote kwa jumla yake ni haramu. Amelaaniwa mwenye kutengeneza picha. Ni moja katika watu watakaopata adhabu kali siku ya Qiyaamah. Ni kipi kinachoitoa simu ndani ya hili? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameharamisha picha kabisa kwa njia yoyote ile, sawa ikiwa ni simu, camera, mkono, kuchora n.k. Ameharamisha uharamu wa moja kwa moja. Ni nani anayemuwekea Istithnaa´ Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?
Wanachuoni wameweka Istithnaa´ katika hali ya dharurah. Mtu akihitajia picha kwa ajili ya dharurah anaruhusiwa kwa ajili ya dharurah. Allaah (Ta´ala) Amesema:
وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ
“… Amekwishakupambanua kwenu yale aliyokuharamishieni kwenu isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura.” (06:119)
Ama aina ya picha zingine zote ni haramu na haijuzu isipokuwa kwa dharurah tu na iwe kwa kiasi cha dharurah tu. Hili ndilo limeruhusiwa na limeruhusiwa kwa ajili ya dharurah tu.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-10-15.mp3
- Imechapishwa: 19/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
41. Maovu ya kwanza: Kutundika picha
1- Kutundika picha Jambo la kwanza: Kutundika picha ukutani, sawa ziwe zenye kiwiliwili cha mwanaadamu au zisizokuwa na kiwiliwili cha mwanaadamu, zenye kivuli au zisiwe na kivuli, zilizochorwa kwa mkono au zilizotengenezwa kutumia vifaa vya kisasa, yote hayo hayajuzu na ni wajibu kwa yule mwenye kuweza kuyaondosha na asipoweza kuyaondosha…
In "Aadaab-uz-Zifaaf"
Kupiga picha kwa kutumia video camera
Swali: Ni ipi hukumu ya kuchukua picha kwa video camera? Je, hilo linaingia katika kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Allaah awalaani watengeneza picha"? Jibu: Ndio, inaingia. Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jumla: "Allaah awalaani watengeneza picha." "Kila mtengeneza picha ni Motoni." Hakukuvuliwa kitu. Picha…
In "Da´wah kwa mapicha na michoro"
Kuhifadhi picha ni jambo halijuzu
Swali: Ni ipi hukumu ya kuhifadhi picha za kivuli pamoja na kuzingatia kwamba mtu hakuzitundika juu ya kuta na amezihifadhi tu ndani ya albamu? Jengine ni kwamba hakuzipiga kwa ajili ya maadhimisho, lakini ni kwa ajili ya kumbukumbu. Jibu: Kuhifadhi picha hizi ni jambo halijuzu. Hilo ni kwa sababu kuhifadhi…
In "Ibn ´Uthaymiyn kuhusu picha"