“Picha ni kivuli tu na haina uharamu wowote”

Swali: Ni ipi hukumu ya picha kwa kutumia camera ya simu kwa kuwa baadhi ya watu wanasema kuwa ni kivuli tu na hilo halina uharamu wowote? Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Haina uharamu wowote kwake yeye. Ama kwa mujibu wa Sunnah na dalili picha zote kwa jumla yake ni haramu. Amelaaniwa mwenye kutengeneza picha. Ni moja katika watu watakaopata adhabu kali siku ya Qiyaamah. Ni kipi kinachoitoa simu ndani ya hili? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameharamisha picha kabisa kwa njia yoyote ile, sawa ikiwa ni simu, camera, mkono, kuchora n.k. Ameharamisha uharamu wa moja kwa moja. Ni nani anayemuwekea Istithnaa´ Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Wanachuoni wameweka Istithnaa´ katika hali ya dharurah. Mtu akihitajia picha kwa ajili ya dharurah anaruhusiwa kwa ajili ya dharurah. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

“… Amekwishakupambanua kwenu yale aliyokuharamishieni kwenu isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura.” (06:119)

Ama aina ya picha zingine zote ni haramu na haijuzu isipokuwa kwa dharurah tu na iwe kwa kiasi cha dharurah tu. Hili ndilo limeruhusiwa na limeruhusiwa kwa ajili ya dharurah tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-10-15.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020