Swali: Tumesikia kwa baadhi ya wanaojinasibisha na elimu wakisema kuwa leo hakuna kundi ambalo mtu anaweza kusema kwa kukata kabisa ya kwamba linamuwakilisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mfumo wa Maswahabah zake. Bali makundi ni mengi tu na kila kundi liko karibu na lingine. Ni upi usahihi wa maneno haya?

Jibu: Anayesema haya ni katika Takfiyriyyuun ambao wanawakufurisha watu na kuwapotosha watu.

Kuna kundi – na himdi zote ni za Allaah – halitoacha kuwepo katika ardhi mpaka Qiyaamah kitaposimama. Huyu anaikadhibisha Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anayesema:

“Hakutoacha kuwepo kipote katika Ummah wangu kuwa juu ya haki waziwazi. Hawatowadhuru wale wenye kuwatosa na  kwenda kinyume nao mpaka ije amri ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala).”

Hadiyth inaonyesha kuwa kuna pote litaloendelea kubaki katika haki mpaka Qiyaamah kitapokuja. Huyu anasema kuwa hakuna kundi hata moja liliopo juu ya haki? Ametakasika Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-10-29.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020